Wagalatia 5:4-6
Wagalatia 5:4-6 NENO
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kupitia kwa Torati mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu. Kwa maana, kupitia Roho wa Mungu tunangojea kwa shauku tumaini la haki kwa imani. Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kupitia kwa upendo.