Wagalatia 5:4-6
Wagalatia 5:4-6 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kupitia kwa Torati mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu. Kwa maana, kupitia Roho wa Mungu tunangojea kwa shauku tumaini la haki kwa imani. Kwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kupitia kwa upendo.
Wagalatia 5:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama mnatazamia kufanywa waadilifu kwa njia ya sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu. Kwa upande wetu, lakini, sisi tunangojea kwa matumaini kwa nguvu ya Roho tufanywe waadilifu kwa njia ya imani. Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
Wagalatia 5:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Wagalatia 5:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.