Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wagalatia 2:16-21

Wagalatia 2:16-21 NENO

bado tunajua kwamba mtu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kupitia kwa imani katika Isa Al-Masihi. Hivyo sisi pia, tumemwamini Al-Masihi Isa ili tupate kuhesabiwa haki kupitia kwa imani katika Al-Masihi, wala si kwa matendo ya sheria, kwa sababu kwa kushika sheria hakuna hata mtu mmoja atakayehesabiwa haki. “Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Al-Masihi, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi. Je, ina maana kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha! Lakini ikiwa mimi ninajenga tena kile ambacho nimekwisha kukibomoa, basi ninaonesha kwamba mimi ni mkosaji. Kwa maana mimi kupitia kwa sheria, nimeifia sheria ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu. Siibatilishi neema ya Mungu, kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kupitia kwa Torati, basi Al-Masihi alikufa bure!”