Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 42:15-20

Ezekieli 42:15-20 NEN

Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka: Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa 500 Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa 500 na upana wa dhiraa 500, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ezekieli 42:15-20