Ezekieli 42:15-20
Ezekieli 42:15-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya yule mtu kulipima eneo la ndani la nyumba ya Mwenyezi-Mungu, alinitoa nje kupitia lango la mashariki na kulipima eneo la nje. Aliuchukua ule ufito wake wa kupimia na kuupima upande wa mashariki, nao ulikuwa mita 250. Akaupima upande wa kaskazini kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250. Kisha akaupima upande wa kusini kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250. Kisha akageuka na kupima upande wa magharibi kwa kutumia ufito wake, nao ulikuwa mita 250. Hivyo akawa amepima pande zote, nazo zilikuwa mita 250 kila upande. Ukuta huo ulitenganisha kati ya eneo takatifu na lile la kawaida.
Ezekieli 42:15-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote. Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Akageuka aelekee upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali ambapo ni pa watu wote.
Ezekieli 42:15-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote. Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Akageuka aelekee upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali palipo pa watu wote.
Ezekieli 42:15-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka: Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa 500 Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa 500 na upana wa dhiraa 500, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote.