Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 9:1-7

Kutoka 9:1-7 NENO

Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” Usipowaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, mkono wa Mwenyezi Mungu utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi. Lakini Mwenyezi Mungu ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ” Mwenyezi Mungu akaweka wakati na kusema, “Kesho Mwenyezi Mungu atalitenda hili katika nchi.” Siku iliyofuata Mwenyezi Mungu akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.

Video ya Kutoka 9:1-7