Kutoka 9:1-7
Kutoka 9:1-7 NENO
Ndipo BWANA akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo BWANA, Mungu wa Waebrania, asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” Usipowaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, mkono wa BWANA utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi. Lakini BWANA ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ” BWANA akaweka wakati na kusema, “Kesho BWANA atalitenda hili katika nchi.” Siku iliyofuata BWANA akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.