Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 26:1-14

Kutoka 26:1-14 NENO

“Tengeneza maskani ya Mungu kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane, na upana wa dhiraa nne. Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, navyo vitanzi vyote vielekeane. Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya maskani ya Mungu iwe kitu kimoja. “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Maskani. Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo sawa, yaani urefu wa dhiraa thelathini, na upana wa dhiraa nne. Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya Maskani. Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia za hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaning’inizwa upande wa nyuma wa maskani ya Mungu. Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaning’inia pande zote za Maskani ili kuifunika. Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.