Kumbukumbu 7:6-10
Kumbukumbu 7:6-10 NENO
kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa BWANA Mungu wako. BWANA Mungu wako amekuchagua kutoka mataifa yote duniani uwe taifa lake, hazina yake ya pekee. BWANA hakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote. Lakini ni kwa sababu BWANA aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri. Basi ujue kwamba BWANA Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. Lakini kwa wale wanaomchukia atawalipiza kwenye nyuso zao kwa maangamizi; hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao wale wamchukiao.