Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 6:20-25

Kumbukumbu 6:20-25 NENO

Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuagiza wewe?” Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Mwenyezi Mungu alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Machoni petu, Mwenyezi Mungu alitenda ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno dhidi ya Misri, na dhidi ya Farao na nyumba yake yote. Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupatia nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo. Mwenyezi Mungu akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo. Tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”