Kumbukumbu la Sheria 6:20-25
Kumbukumbu la Sheria 6:20-25 Biblia Habari Njema (BHN)
“Siku zijazo, watoto wenu wakiwauliza, ‘Nini maana ya maamuzi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, aliwaamuru kutenda?’ Nyinyi mtawajibu hivi: ‘Sisi tulikuwa watumwa wa Farao, mfalme wa Misri, na Mwenyezi-Mungu akatuokoa kwa mkono wake wenye nguvu. Kwa macho yetu wenyewe tulimwona akifanya ishara na miujiza na mambo ya kutisha na ya ajabu dhidi ya Wamisri, mfalme wao na wakuu wake. Alitutoa Misri, akatuleta hapa na kutupa nchi hii, kama alivyoapa kwamba atawapa babu zetu. Basi, Mwenyezi-Mungu alituamuru kuzitii kanuni hizi zote na kumcha kwa faida yetu wenyewe; apate kutulinda daima kama hivi leo. Tena tutakuwa waadilifu kama tukitimiza kwa uangalifu amri hizi zote mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru’.

Kumbukumbu la Sheria 6:20-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, Ni nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; BWANA akaonesha ishara na maajabu makubwa na mazito, juu ya Misri, Farao, na nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia babu zetu. BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo. Tena itakuwa haki kwetu, tukizingatia kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.
Kumbukumbu la Sheria 6:20-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; BWANA akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu. BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo. Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.
Kumbukumbu la Sheria 6:20-25 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuagiza wewe?” Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Mwenyezi Mungu alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Machoni petu, Mwenyezi Mungu alitenda ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno dhidi ya Misri, na dhidi ya Farao na nyumba yake yote. Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupatia nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo. Mwenyezi Mungu akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo. Tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”