Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 33:1-5

Kumbukumbu 33:1-5 NENO

Hii ndiyo baraka Musa mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. Alisema: “Mwenyezi Mungu alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka miteremko ya mlima wake. Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu, watakatifu wako wote wamo mkononi mwako. Miguuni pako wote wanasujudu, na kutoka kwako wanapokea mafundisho, sheria ile Musa aliyotupatia sisi, tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni wakati viongozi wa watu walipokusanyika, pamoja na makabila ya Israeli.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha