Kumbukumbu la Sheria 33:1-5
Kumbukumbu la Sheria 33:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao. Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja.
Kumbukumbu la Sheria 33:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Hii ndiyo baraka ambayo Mose, mtu wa Mungu aliwatakia Waisraeli kabla ya kufariki kwake. Alisema: Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia. Mwenyezi-Mungu aliwapenda watu wake; na huwalinda watakatifu wake wote. Hivyo, malaika wake walifuata nyayo zake, na kupata maagizo kutoka kwake. Mose alituamuru tutii sheria; kitu cha thamani kuu cha taifa letu. Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli, wakati viongozi wao walipokutana, na makabila yote yalipokusanyika.

Kumbukumbu la Sheria 33:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao. Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja.
Kumbukumbu la Sheria 33:1-5 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Hii ndiyo baraka Musa mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. Alisema: “Mwenyezi Mungu alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka miteremko ya mlima wake. Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu, watakatifu wako wote wamo mkononi mwako. Miguuni pako wote wanasujudu, na kutoka kwako wanapokea mafundisho, sheria ile Musa aliyotupatia sisi, tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni wakati viongozi wa watu walipokusanyika, pamoja na makabila ya Israeli.