Kumbukumbu 27:1-10
Kumbukumbu 27:1-10 NENO
Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi anayowapa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na myapake chokaa. Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi anayowapa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, nchi inayotiririka maziwa na asali, kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, na myapake chokaa. Huko mjengeeni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake. Jengeni madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.” Kisha Musa na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Mtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”