Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 5:10-17

Amosi 5:10-17 NENO

mnamchukia yule akemeaye mahakamani, na kumdharau yule ambaye husema kweli. Mnamgandamiza maskini na kumlazimisha awape nafaka. Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari, hamtaishi ndani yake; ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, hamtakunywa divai yake. Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu. Mmewadhulumu wenye haki na kupokea rushwa na kuzuia haki ya maskini mahakamani. Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza nyakati kama hizo, kwa kuwa nyakati ni mbaya. Tafuteni mema, wala si mabaya, ili mpate kuishi. Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo yupo nanyi. Yachukieni maovu, yapendeni mema; dumisheni haki mahakamani. Yamkini Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, atawahurumia mabaki ya Yusufu. Kwa hiyo hili ndilo Bwana, yeye Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asemalo: “Kutakuwa na maombolezo barabarani zote, na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza. Kutakuwa na kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, kwa kuwa nitapita kati yenu,” asema Mwenyezi Mungu.