Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

3 Yohana 1:1-5

3 Yohana 1:1-5 NEN

Mzee: Kwa Gayo rafiki yangu, nimpendaye katika kweli. Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo. Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli. Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako.