Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo 4:14-22

2 Timotheo 4:14-22 NEN

Aleksanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda. Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba. Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen. Wasalimu Prisila na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo. Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa. Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote. Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.