Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Petro 1:2-11

2 Petro 1:2-11 NENO

Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi katika kumjua Mungu na Isa Bwana wetu. Uweza wake wa uungu umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya uungu, na kuokoka kutoka upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya. Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa; katika utauwa, upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu, upendo. Kwa maana haya yakiwa ndani yenu kwa wingi na kuzidi kuongezeka, yatawasaidia kutokosa bidii wala kutokuzaa matunda katika kumjua Bwana wetu Isa Al-Masihi. Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya, haoni mbali na ni kipofu, naye amesahau kwamba ametakaswa kutoka dhambi zake za zamani. Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuthibitisha wito wenu na uteule wenu. Kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe, na mtajaliwa kwa ukarimu mwingi kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Isa Al-Masihi.