Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo Utangulizi

Utangulizi
Nyaraka za 1 na 2 Timotheo na ule wa Tito zinatambuliwa kama nyaraka za kichungaji zilizoandikwa na Paulo. Alimwandikia Timotheo msaidizi wake, ambaye alikuwa amemwacha huko Efeso kusahihisha matatizo kadhaa kuhusu mwenendo wa makundi ya waumini, uongozi wa makundi hayo, na mambo yaliyowahusu waumini binafsi. Paulo aliandika ili kumpa Timotheo maagizo kuhusu mambo haya, ili kila kundi la waumini lifanye kazi yake vyema. Aliandika pia kumtia moyo Timotheo asichoke katika maisha yake ya mfuasi wa Al-Masihi, bali aishi maisha ya ukamilifu kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Timotheo alizaliwa huko Listra. Baba yake alikuwa Myunani, naye mama yake Myahudi ambaye alimfundisha Maandiko tangu utoto. Paulo alipofika Listra katika safari yake ya pili kueneza Injili, alimchagua Timotheo ambaye alishirikiana naye hadi mwisho wa huduma yake.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kumtia moyo na kumpa maelekezo Timotheo, ambaye alikuwa kiongozi mchanga, kuhusu utaratibu wa makundi ya waumini kwa jumla, imani na maadibisho.
Mahali
Pengine Filipi.
Tarehe
Mnamo 64 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo na Timotheo.
Wazo Kuu
Umuhimu wa kuwa na imani sahihi, mwenendo mnyofu, na pia uadilifu.
Mambo Muhimu
Kumwelekeza Timotheo kuhusu sifa na wajibu wa viongozi mbalimbali katika makundi ya waumini, na kumpa mwongozo katika wajibu wake wa kichungaji.
Yaliyomo
Salamu, na maonyo dhidi ya walimu wa uongo (1:1-20)
Maagizo kuhusu maombi (2:1-15)
Sifa zinazowapasa viongozi wa makundi ya waumini (3:1-16)
Maonyo na huduma (4:1–5:25)
Huduma ya mfuasi wa Al-Masihi, na maagizo kwa Timotheo (6:1-21).

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia