1 Petro Utangulizi
Utangulizi
Mtume Petro ni mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili wa Isa. Aliandikia waraka huu kwa wafuasi wa Al-Masihi wa Kiyahudi waliotawanyika huko sehemu ya Asia Ndogo. Waraka huu unaonesha kwamba waumini walikuwa wanakabiliwa na dhiki na mateso. Lengo lake lilikuwa kuwafariji waumini walioishi jimbo la Asia, kwani katika kipindi hiki cha miaka ya sitini ya karne ya kwanza, utawala wa Rumi chini ya Nero ulianza kuwatesa wafuasi wa Al-Masihi.
Kwa wale waliokuwa wakifikiria kurudia imani yao ya Kiyahudi ili kuepuka mateso, anawaambia kuwa sasa jumuiya ya waumini ndiyo ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki yake Mwenyezi Mungu. Hivyo mawazo ya kurejea imani ya Kiyahudi hayana faida yoyote. Kisha Petro anatoa mfano wa Al-Masihi na jinsi alivyopata mateso, na anawakumbusha waumini kuwa wao pia hawana budi kupata mateso. Mwishowe, Petro anatoa maagizo kwa vikundi mbalimbali vya wafuasi wa Al-Masihi.
Mwandishi
Mtume Petro.
Kusudi
Kuwatia moyo wafuasi wa Al-Masihi kusimama dhabiti katika mateso yote, na kuwa imara katika neema ya Mwenyezi Mungu.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 63 B.K.
Wahusika Wakuu
Petro, Silvano, na Marko.
Wazo Kuu
Hata kama tutauawa kwa ajili ya imani, tushikilie imani yetu. Mwenyezi Mungu anafahamu yote yanayotendeka, na katika mpango wake wa milele, hatimaye mambo yote yatakamilika kwa utukufu wake.
Mambo Muhimu
Petro anaonesha kwamba mateso ni sehemu ya maisha ya wafuasi wa Al-Masihi, na kwamba Mwenyezi Mungu ameandaa thawabu zisizoharibika kwa wote wanaomwamini. Pia anaonesha tumaini la wakati wa mwisho kuwa jambo la kumtia moyo muumini katika mateso.
Yaliyomo
Salamu, utukufu wa wokovu wa Al-Masihi (1:1-25)
Utiifu wa mfuasi wa Al-Masihi (2:1-25)
Maisha yampasayo mfuasi wa Al-Masihi (3:1–4:11)
Huduma ya wafuasi wa Al-Masihi, na salamu za mwisho (4:12–5:14).
Iliyochaguliwa sasa
1 Petro Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.