Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 4:1-20

1 Wafalme 4:1-20 NEN

Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki; Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani; Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani; Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme; Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha. Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu; Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani; Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake); Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni); Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu; Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba); Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu; Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni); Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi; Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari; Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini; Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo. Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.