Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 4:1-20

1 Wafalme 4:1-20 Biblia Habari Njema (BHN)

Solomoni alikuwa mfalme wa nchi yote ya Israeli, na wafuatao walikuwa baadhi ya maofisa wake wa vyeo vya juu: Azaria, mwana wa Sadoki, alikuwa kuhani. Elihorefu na Ahiya wana wa Shausha, walikuwa makatibu; Yehoshafati mwana wa Ahiludi, alikuwa mweka kumbukumbu za habari. Benaya mwana wa Yehoyada, alikuwa jemadari wa jeshi; nao Sadoki na Abiathari, walikuwa makuhani. Azaria mwana wa Nathani, alikuwa ofisa mkuu tawala; kuhani Zabudi mwana wa Nathani, alikuwa rafiki wa mfalme. Ahishari alikuwa mkuu wa ikulu na Adoniramu mwana wa Abda, alikuwa msimamizi wa kazi za kulazimishwa. Solomoni aliteua maofisa tawala kumi na wawili kwa nchi nzima ya Israeli. Hao walipewa jukumu la kutafuta chakula kwa ajili ya mfalme na nyumba yake; kila mmoja wao alileta chakula kutoka mkoani kwake kwa mwezi mmoja kila mwaka. Haya ndiyo majina ya hao maofisa tawala: Ben-huri alisimamia sehemu ya milima ya Efraimu; Ben-dekeri alisimamia miji ya Makai, Shaalbimu, Beth-shemeshi na Elon-beth-hanani. Ben-hesedi alisimamia mji wa Arubothi, alisimamia pia Soko na nchi yote ya Heferi. Ben-abinadabu, mume wa Tafathi, binti Solomoni, alisimamia kanda yote ya Nafath-dori. Baana, mwana wa Ahiludi, alisimamia miji ya Taanaki, Megido, na sehemu yote ya Beth-sheani iliyo karibu na mji wa Zarethi, kusini ya mji wa Yezreeli, na kutoka Beth-sheani mpaka miji ya Abel-mehola, na hata kupita mji wa Yokmeamu. Ben-geberi, alisimamia mji wa Ramoth-gileadi pamoja na vijiji vya Gileadi vilivyokuwa chini ya Yairi, mwana wa Manase; pia alisimamia mkoa wa Argobu ulioko Bashani; yote jumla ilikuwa miji mikubwa sitini iliyozungushiwa kuta na kuwekwa fito za shaba malangoni. Ahinadabu, mwana wa Ido, alisimamia jimbo la Mahanaimu. Ahimaasi, mumewe Basemathi, binti Solomoni, alisimamia wilaya ya Naftali. Baana mwana wa Hushai, alisimamia wilaya ya Asheri na Bealothi. Yehoshafati mwana wa Parua, alisimamia wilaya ya Isakari. Shimei, mwana wa Ela, alisimamia wilaya ya Benyamini. Geberi, mwana wa Uri, alisimamia wilaya ya Gileadi, ambayo hapo awali ilitwaliwa na Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani. Licha ya hawa kumi na wawili, palikuwa na mkuu mmoja aliyesimamia nchi nzima ya Yuda. Watu wa Yuda na wa Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani, nao walikuwa wakila, wakinywa, na kufurahi.

1 Wafalme 4:1-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote. Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani, Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe; na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa jemadari wa jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme. Na Ahishari alikuwa mkuu wa kasri; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa msimamizi wa shokoa. Sulemani alikuwa na maafisa tawala kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula. Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu. Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Beth-shemeshi na Elon-beth-hanani. Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi. Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake. Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu. Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba. Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu. Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani. Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi. Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari. Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini. Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa mkuu pekee katika nchi hiyo. Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.

1 Wafalme 4:1-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote. Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani, Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe; na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; na Azaria mwana wa Nathani alikuwa juu ya maakida; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki wake mfalme. Na Ahishari alikuwa juu ya nyumba; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa juu ya shokoa. Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula. Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu. Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Bethshemeshi na Elon-beth-hanani. Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi. Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake. Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu. Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba. Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu. Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani. Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi. Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari. Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini. Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa akida wa pekee katika nchi hiyo. Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.

1 Wafalme 4:1-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu: Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki; Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani; Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; Sadoki na Abiathari: makuhani; Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme; Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha. Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. Majina yao ni haya: Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu; Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani; Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake); Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni); Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu; Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba); Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu; Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni); Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi; Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari; Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini; Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo. Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi.