1 Wakorintho 9:19-23
1 Wakorintho 9:19-23 NENO
Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadiri iwezekanavyo. Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa watu wale walio chini ya Torati, nilikuwa kama aliye chini ya Torati (ingawa mimi siko chini ya Torati), ili niweze kuwapata wale walio chini ya Torati. Kwa watu wasio na Torati nilikuwa kama asiye na Torati (ingawa siko huru mbali na Torati ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Al-Masihi), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria. Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao. Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake.