1 Wakorintho 9:19-23
1 Wakorintho 9:19-23 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadiri iwezekanavyo. Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa watu wale walio chini ya Torati, nilikuwa kama aliye chini ya Torati (ingawa mimi siko chini ya Torati), ili niweze kuwapata wale walio chini ya Torati. Kwa watu wasio na Torati nilikuwa kama asiye na Torati (ingawa siko huru mbali na Torati ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Al-Masihi), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria. Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao. Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake.
1 Wakorintho 9:19-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo. Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini ya sheria, nimejiweka chini ya sheria kwao, ili niwapate hao walio chini ya sheria. Na kwa wale walio nje ya sheria, naishi kama wao, nje ya sheria, ili niwapate hao walio nje ya sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo. Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia. Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, nipate kushiriki baraka zake.
1 Wakorintho 9:19-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nilijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe siko chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria nilikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. Kwa wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
1 Wakorintho 9:19-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.