Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati Utangulizi

Utangulizi
Jina hili la kitabu “Mambo ya Nyakati” linaweza likafuatiliwa hadi kwa Yerome ambaye alilitumia katika tafsiri ya Kilatini ya Maandiko Matakatifu, yaani “Vulgate.” Jina la kitabu hiki katika Kiyunani, “Mambo Yaliyorukwa,” linaonesha ile hali ya watafsiri wa Maandiko Matakatifu katika “Septuagint” kwamba mambo yaliyomo katika vitabu hivi kimsingi yalikuwa mambo ya nyongeza yaliyokuwa yameachwa na vitabu vya Samweli na Wafalme.
Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati viliandikwa kwa ajili ya watu waliorudi Israeli kutoka utumwani, baada ya kutekwa na kupelekwa Babeli, ili kuwakumbusha kwamba walikuwa wa ukoo wa ufalme wa Daudi, na kwamba wao walikuwa watu wateule wa Mwenyezi Mungu.
Mwandishi
Mapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.
Kusudi
Kuunganisha watu wa Mwenyezi Mungu, kufuatilia ukoo wa Daudi, na kufundisha watu sala iliyo ya kweli ambayo ndiyo hitaji kubwa katika maisha ya mtu binafsi na taifa pia.
Mahali
Yerusalemu, na katika Hekalu.
Tarehe
Kama mwaka wa 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Daudi na Sulemani.
Wazo Kuu
Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kinaelezea kwa kifupi historia na koo za Waisraeli tangu Adamu hadi kifo cha Mfalme Sauli. Sehemu ya kitabu iliyobaki inaeleza habari za Mfalme Daudi.
Mambo Muhimu
Kuelezea historia ya vizazi vya Israeli, na habari kumhusu Mfalme Daudi na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, na kuletwa kwa Sanduku la Agano huko Yerusalemu kama chanzo cha sala ya kweli.
Yaliyomo
Orodha ya Vizazi (1:1–9:44)
Orodha ya nasaba za mababa wa taifa
Makabila ya Israeli
Kurudi kutoka utumwani Babeli.
Utawala wa Daudi (10:1–29:30)
Daudi afanyika mfalme juu ya Israeli yote
Daudi alirudisha Sanduku la Mwenyezi Mungu Yerusalemu
Majeshi ya Daudi yajinufaisha
Daudi aandaa kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia