Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 3

3
Wana wa Daudi
1Hawa walikuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:
Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;
wa pili, Danieli ambaye mama yake aliitwa Abigaili wa Karmeli;
2wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake aliitwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;
wa nne, Adoniya, ambaye mama yake aliitwa Hagithi;
3wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake aliitwa Abitali;
wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
4Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.
Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na tatu, 5nao hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:
mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia wana wanne: Shamua#3:5 au Shimea, Shobabu, Nathani na Sulemani.
6Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, 7Noga, Nefegi, Yafia, 8Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.
9Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.
Wafalme wa Yuda
10Mwana wa Sulemani alikuwa Rehoboamu,
mwanawe huyo alikuwa Abiya,
mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,
mwanawe huyo alikuwa Asa,
11mwanawe huyo alikuwa Yehoramu,
mwanawe huyo alikuwa Ahazia,
mwanawe huyo alikuwa Yoashi,
12mwanawe huyo alikuwa Amazia,
mwanawe huyo alikuwa Azaria,
mwanawe huyo alikuwa Yothamu,
13mwanawe huyo alikuwa Ahazi,
mwanawe huyo alikuwa Hezekia,
mwanawe huyo alikuwa Manase,
14mwanawe huyo alikuwa Amoni
na mwanawe huyo alikuwa Yosia.
15Wana wa Yosia walikuwa:
Yohanani mzaliwa wake wa kwanza,
Yehoyakimu mwanawe wa pili,
wa tatu Sedekia,
wa nne Shalumu.
16Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:
Yekonia mwanawe,
na Sedekia.
Ukoo wa kifalme baada ya uhamisho
17Hawa walikuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:
Shealtieli mwanawe, 18Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
19Wana wa Pedaya walikuwa:
Zerubabeli na Shimei.
Wana wa Zerubabeli walikuwa:
Meshulamu na Hanania. Shelomithi alikuwa dada yao. 20Kulikuwa na wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.
21Wazao wa Hanania walikuwa:
Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
22Wazao wa Shekania:
Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.
23Wana wa Nearia walikuwa:
Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.
24Wana wa Elioenai walikuwa:
Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nyakati 3: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia