Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 10:1-13

1 Nyakati 10:1-13 NENO

Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa. Wafilisti wakawafuatilia Sauli na wanawe kwa karibu, na wakawaua Yonathani, Abinadabu, na Malki-Shua. Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi. Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa. Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote. Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaenda na kuyamiliki. Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, na wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni. Wakazi wote wa Yabesh-Gileadi waliposikia yale Wafilisti waliyomtendea Sauli, mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni ulio Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba. Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu. Hakulishika neno la Mwenyezi Mungu, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi