1
Mwanzo 22:14
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ibrahimu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Hadi leo inasemekana, “Katika mlima wa Mwenyezi Mungu itapatikana.”
Linganisha
Chunguza Mwanzo 22:14
2
Mwanzo 22:2
Kisha Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, uende nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima nitakaokuambia.”
Chunguza Mwanzo 22:2
3
Mwanzo 22:12
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Chunguza Mwanzo 22:12
4
Mwanzo 22:8
Ibrahimu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.
Chunguza Mwanzo 22:8
5
Mwanzo 22:17-18
Hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga wa pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”
Chunguza Mwanzo 22:17-18
6
Mwanzo 22:1
Baadaye Mungu akamjaribu Ibrahimu. Akamwambia, “Ibrahimu!” Ibrahimu akamjibu, “Mimi hapa.”
Chunguza Mwanzo 22:1
7
Mwanzo 22:11
Lakini malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Ibrahimu! Ibrahimu!” Akajibu, “Mimi hapa.”
Chunguza Mwanzo 22:11
8
Mwanzo 22:15-16
Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita Ibrahimu kutoka mbinguni mara ya pili, akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Mwenyezi Mungu, kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee
Chunguza Mwanzo 22:15-16
9
Mwanzo 22:9
Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaka mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni.
Chunguza Mwanzo 22:9
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video