1
Mathayo 16:24
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
Linganisha
Chunguza Mathayo 16:24
2
Mathayo 16:18
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kuwashinda.
Chunguza Mathayo 16:18
3
Mathayo 16:19
Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
Chunguza Mathayo 16:19
4
Mathayo 16:25
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.
Chunguza Mathayo 16:25
5
Mathayo 16:26
Kwa maana itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Chunguza Mathayo 16:26
6
Mathayo 16:15-16
Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu aliye hai.”
Chunguza Mathayo 16:15-16
7
Mathayo 16:17
Naye Isa akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.
Chunguza Mathayo 16:17
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video