1
Mithali 15:1
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira.
Linganisha
Chunguza Mithali 15:1
2
Mithali 15:33
Kumcha Mwenyezi Mungu humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.
Chunguza Mithali 15:33
3
Mithali 15:4
Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho.
Chunguza Mithali 15:4
4
Mithali 15:22
Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri, bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa.
Chunguza Mithali 15:22
5
Mithali 15:13
Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho.
Chunguza Mithali 15:13
6
Mithali 15:3
Macho ya Mwenyezi Mungu yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema.
Chunguza Mithali 15:3
7
Mithali 15:16
Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.
Chunguza Mithali 15:16
8
Mithali 15:18
Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.
Chunguza Mithali 15:18
9
Mithali 15:28
Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.
Chunguza Mithali 15:28
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video