1
Mithali 14:12
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
Linganisha
Chunguza Mithali 14:12
2
Mithali 14:30
Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa.
Chunguza Mithali 14:30
3
Mithali 14:29
Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonesha upumbavu.
Chunguza Mithali 14:29
4
Mithali 14:1
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Chunguza Mithali 14:1
5
Mithali 14:26
Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
Chunguza Mithali 14:26
6
Mithali 14:27
Kumcha Mwenyezi Mungu ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
Chunguza Mithali 14:27
7
Mithali 14:16
Mtu mwenye hekima humcha Mwenyezi Mungu na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.
Chunguza Mithali 14:16
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video