1
Marko 10:45
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Linganisha
Chunguza Marko 10:45
2
Marko 10:27
Isa akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”
Chunguza Marko 10:27
3
Marko 10:52
Isa akamwambia, “Nenda zako, imani yako imekuponya.” Mara akapata kuona, akamfuata Isa njiani.
Chunguza Marko 10:52
4
Marko 10:9
Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
Chunguza Marko 10:9
5
Marko 10:21
Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”
Chunguza Marko 10:21
6
Marko 10:51
Isa akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.”
Chunguza Marko 10:51
7
Marko 10:43
Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu
Chunguza Marko 10:43
8
Marko 10:15
Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”
Chunguza Marko 10:15
9
Marko 10:31
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Chunguza Marko 10:31
10
Marko 10:6-8
Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke’. ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja.
Chunguza Marko 10:6-8
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video