Marko 10:6-8
Marko 10:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.
Marko 10:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwaumba mwanamume na mwanamke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Marko 10:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Marko 10:6-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja.