Zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, binti Abihaili, mjomba wake), Esta hakutaka vitu zaidi ya vile Hegai, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake, alikuwa amemshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.