1
Wakolosai 2:6-7
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Hivyo basi, kama vile mlivyompokea Al-Masihi Isa kuwa Bwana, endeleeni kukaa ndani yake, mkijikita na kujengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.
Linganisha
Chunguza Wakolosai 2:6-7
2
Wakolosai 2:8
Chungeni mtu yeyote asiwafanye ninyi mateka kwa elimu batili na madanganyo matupu, yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya ulimwengu badala ya Al-Masihi.
Chunguza Wakolosai 2:8
3
Wakolosai 2:13-14
Mlipokuwa wafu katika dhambi zenu na kutokutahiriwa katika asili yenu ya dhambi, Mungu aliwafanya mwe hai pamoja na Al-Masihi. Alitusamehe dhambi zetu zote, baada ya kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili, pamoja na maagizo yake. Aliiondoa isiwepo tena, akaigongelea kwenye msalaba wake.
Chunguza Wakolosai 2:13-14
4
Wakolosai 2:9-10
Maana utimilifu wote wa Mungu unakaa ndani ya Al-Masihi katika umbile la mwili wa kibinadamu, nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, aliye mkuu juu ya kila nguvu na kila mamlaka.
Chunguza Wakolosai 2:9-10
5
Wakolosai 2:16-17
Basi, mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwezi Mwandamo au siku ya Sabato. Hizi zilikuwa kivuli cha mambo yajayo; lakini uhalisi unapatikana kwa Al-Masihi.
Chunguza Wakolosai 2:16-17
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video