Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupatia sisi tuliomwamini Bwana Isa Al-Masihi, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?”
Waliposikia haya hawakuwa na lingine la kupinga. Nao wakamsifu Mungu, wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”