1
2 Nyakati 20:15
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Akasema: “Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mnaoishi Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu.
Linganisha
Chunguza 2 Nyakati 20:15
2
2 Nyakati 20:17
Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Mwenyezi Mungu atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja nanyi.’ ”
Chunguza 2 Nyakati 20:17
3
2 Nyakati 20:12
Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.”
Chunguza 2 Nyakati 20:12
4
2 Nyakati 20:21
Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa kuwa fadhili zake zadumu milele.”
Chunguza 2 Nyakati 20:21
5
2 Nyakati 20:22
Walipoanza kuimba na kusifu, Mwenyezi Mungu akaweka waviziaji dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa.
Chunguza 2 Nyakati 20:22
6
2 Nyakati 20:3
Yehoshafati akaogopa, akaamua kumtafuta Mwenyezi Mungu, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga.
Chunguza 2 Nyakati 20:3
7
2 Nyakati 20:9
‘Kama maafa yakitujia, ikiwa ni upanga, hukumu, tauni, au njaa, tutasimama mbele zako, mbele ya Hekalu hili ambalo limeitwa kwa Jina lako na kukulilia katika shida yetu, nawe utatusikia na kutuokoa.’
Chunguza 2 Nyakati 20:9
8
2 Nyakati 20:16
Kesho shukeni kukabiliana nao. Watakwea kwa kupandia Genge la Sisi, nanyi mtawakuta mwisho wa bonde, kabla ya Jangwa la Yerueli.
Chunguza 2 Nyakati 20:16
9
2 Nyakati 20:4
Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta.
Chunguza 2 Nyakati 20:4
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video