1 Mose 4
4
Wana wa Adamu.
1Adamu akamtambua mkewe Ewa, akapata mimba; kisha akamzaa Kaini, akasema: Nimepata mwanamume kwa Bwana. 2Tena akamzaa ndugu yake Abeli; naye Abeli akawa mchunga kondoo, lakini Kaini akawa mlima shamba. 3Siku zilipopita, Kaini akampelekea Bwana mazao ya shamba kuwa kipaji cha tambiko. 4Abeli naye akapeleka malimbuko ya kundi lake yenye manono. Bwana akamtazama Abeli na kipaji chake kwa kupendezwa,#Ebr. 11:4. 5lakini Kaini na kipaji chake hakumtazama. Ndipo, makali ya Kaini yalipowaka moto sana, haata uso wake ukakunjamana. 6Naye Bwana akamwuliza Kaini: Mbona makali yako yamewaka moto? Mbona uso wako umekunjamana? 7Tazama, sivyo hivyo? Ukifanya mema utanielekezea macho; lakini usipofanya mema, ukosaji hulala mlangoni na kukutamani, lakini wewe sharti uushinde!#Gal. 5:17; Rom. 6:12.
Kaini anamwua nduguye Abeli.
8Kisha Kaini akaongea na nduguye Abeli; lakini walipofika shambani, ndipo, Kaini alipomwinukia nduguye Abeli, akamwua.#Yoh. 3:12,15. 9Naye Bwana alipomwuliza Kaini: Ndugu yako Abeli yuko wapi? akajibu: Sijui; je? Mimi ni mlezi wa ndugu yangu? 10Akamwuliza tena; Umefanya nini? Sauti za damu ya ndugu yako zinanililia huko nchini!#Sh. 9:13; Mat. 23:35; Ebr. 12:24. 11Sasa wewe umeapizwa katika nchi hii iliyoasama kuipokea damu ya ndugu yako mkononi mwako. 12Utakapolima shamba, halitakupa tena liyawezayo kuzaa, utakuwa ukikimbiakimbia na kutangatanga katika nchi. 13Ndipo, Kaini alipomwambia Bwana: Manza zangu ni kubwa, haziwezekani kuondolewa. 14Tazama, umenifukuza leo hivi katika nchi hii, nami nitajificha, nisiuone uso wako tena, niwe mwenye kukimbiakimbia na kutangatanga katika nchi hii, kisha atakayeniona ataniua.#Iy. 15:20-24. 15Lakini Bwana akamwambia: Atakayemwua Kaini atalipizwa mra saba. Kisha Bwana akamtia Kaini alama, kila atakayemwona asimwue. 16Kisha Kaini akatoka machoni pa Bwana, akaenda kukaa katika nchi ya Nodi iliyoko ng'ambo ya Edeni.
Kizazi cha Kaini.
17Kaini akamtambua mkewe, akapata mimba, kisha akamzaa Henoki. Naye Kaini alipojenga mji akauita huo mji kwa jina la mwanawe Henoki. 18Nenoki akapata mwana, ndiye Iradi, naye Iradi akamzaa Mehuyaeli, naye Mehuyaeli akamzaa Metusaeli, naye Metusaeli akamzaa Lameki. 19Lameki akajichukulia wake wawili, jina lake wa kwanza ni Ada, jina lake wa pili ni Sila. 20Ada akamzaa Yabali; yeye ndiye baba yao wanaokaa mahemani na kufuga nyama. 21Nalo jina la nduguye ni Yubali, yeye ndiye baba yao wapiga mazeze na mazomari. 22Sila naye akamzaa Tubalkaini, naye alikuwa mhunzi aliyejua kufua vyombo vyote vya shaba na vya chuma; naye umbu lake Tubalkaini alikuwa Nama. 23Lameki akawaambia wakeze Ada na Sila:
Isikieni sauti yangu, ninyi wakeze Lameki!
Yategeni masikio yenu, myasikie maneno yangu!
Nimeua mtu, kwani aliniumiza,
naye ni kijana, lakini alinitia mavilio.
24Kaini akilipizwa kisasi mara saba,
Lameki na alipizwe kisasi mara sabini na saba.#1 Mose 4:15; Mat. 18:21-22.
Kuzaliwa kwake Seti.
25Adamu alipomtambua mkewe tena, akazaa mwana wa kiume, akamwita jina lake Seti (Pato), kwani alisema: Mungu amenipatia mzao mwingine mahali pake Abeli, kwa kuwa kaini alimwua. 26Seti naye alipozaliwa mwana akamwita jina lake Enosi. Siku hizo ndipo, watu walipoanza kulitambikia Jina la Bwana.#1 Mose 12:8.
Zvasarudzwa nguva ino
1 Mose 4: SRB37
Sarudza vhesi
Pakurirana nevamwe
Sarudza zvinyorwa izvi
Unoda kuti zviratidziro zvako zvichengetedzwe pamidziyo yako yose? Nyoresa kana kuti pinda
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.