1 Mose 3
3
Kosa la kwanza.
1Nyoka alikuwa mjanja kuliko nyama wote wa porini, Bwana Mungu aliowafanya. Naye akamwambia mwanamke: Kumbe Mungu amewakataza kuila miti yote iliyomo humu shambani?#Ufu. 12:9. 2Lakini mwanamke akamwambia nyoka: Tunayala matunda ya miti iliyomo humu shambani;#1 Mose 2:16. 3lakini matunda ya mti huu katikati ya shamba Mungu ametuambia: Msiyale! Msiyaguse, msipate kufa!#1 Mose 2:17. 4Ndipo, nyoka alipomwambia mwanamke: kufa hamtakufa kabisa.#Yoh. 8:44. 5Kwani Mungu anajua, ya kuwa siku, mtakapoula, macho yenu yatafumbuliwa, mwe kama Mungu mkijua mema na mabaya. 6Mwanamke alipoutazama huo mti akauona kuwa mwema wa kula, hata wa kuyapendeza macho, tena akauona, ya kuwa unapasa kutamaniwa kwa kuerevusha; ndipo, alipochuma tunda mojamoja, akala, akampa hata mumewe, naye akala.#Yak. 1:14; 1 Tim. 2:14. 7Ndipo, macho yao wote wawili yalipofumbuliwa, wakatambua, ya kuwa wako uchi; kwa hiyo wakashona majani ya mkuyu, wakayatumia ya kujifunga viunoni.#1 Mose 2:25.
Mapatilizo ya hilo kosa la kwanza.
8Jua lilipokuwa limeponga, wakakisikia kishindo cha Bwana Mungu, akitembea shambani; ndipo, Adamu na mkewe walipojificha kwenye miti ya shamba, Bwana Mungu asiwaone.#Yer. 23:24. 9Bwanaa Mungu akamwita Adamu akisema: Uko wapi? 10Akajibu: Nimekisikia kishindo chako shambani, nikaogopa, kwa kuwa mimi ni mwenye uchi, nikajificha. 11Akasema: Ni nani aliyekuambia, ya kuwa wewe u mwenye uchi? Hukuula ule mti, niliokukataza, usiule? 12Naye Adamu akasema: Huyu mwanamke, uliyonipa kuwa nami, yeye amenipa tunda la mti ule, nikalila. 13Bwana Mungu akamwuliza mwanamke; Mbona umeyafanya hayo? Mwanamke akamwambia: Nyoka amenidanganya, nikala.#2 Kor. 11:3. 14Ndipo, Bwana Mungu alipomwambia nyoka: Kwa kuwa umeyafanya hayo, utakuwa umeapizwa wewe kuliko nyama wote wa nyumbani na wa porini, utajiburura kwa tumbo lako, ule mavumbi siku zako zote za kuwapo.#Yes. 65:25. 15Na niwachochee, mchukizane, wewe na huyu mwanamke, uzao wako na uzao wake, huyo atakuponda kichwa, nawe utamwuma kisigino.#Gal. 4:4; 1 Yoh. 3:8; Ebr. 2:14; Rom. 16:20; Yoh. 14:30; Ufu. 12:17. 16Kisha akamwambia mwanamke: Nitakupatia maumivu mengi, utakapopata mimba, itakuwa kwa machngu mengi, ukizaa watoto; ijapo yawe hivyo, utamtamani mumeo, naye atakutawala.#Ef. 5:22-23; 1 Tim. 2:11-12. 17Adamu naye akamwambia: Kwa kuwa umeiitikia sauti ya mkeo, ukaula ule mti, niliokuagiza kwamba: Usiule! nchi imeapizwa kwa ajili yako, uile na kuona uchungu siku zako zote za kuwapo. 18Itakuoteshea miiba na mibigili, nawe utakula majani ya shambani. 19Kwa jasho la uso wako utakula chakula, mpaka utakaporudi mchangani, kwani ndimo, ulimochukuliwa, kwani ndiwe mavumbi wewe, nayo mavumbi ndiyo, utakayokuwa tena.#2 Tes. 3:10; Mbiu. 12:7.
Kufukuzwa Paradiso.
20Adamu akamwita mkewe jina lake Ewa, kwa kuwa ndiye mama yao wote walio hai. 21Bwana Mungu akamtengenezea Adamu na mkewe ngozi za kuvaa, akawavika. 22Kisha Bwana Mungu akasema: Ninamwona Adamu, ya kuwa amekwisha kuwa kama mwenzetu kwa kujua mema na mabaya; labda sasa ataupeleka mkono wake, achume nayo matunda ya mti wa uzima na kuyala, apate kuwapo kale na kale.#1 Mose 3:5. 23Kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika hilo shamba la Edeni, ailime nchi, alimochukuliwa. 24Ndiyo sababu, aliyomfukuzia Adamu, nao upande wa maawioni kwa jua wa shamba la Edeni akaweka Makerubi wenye panga zimulikazo moto pande zote, wailinde njia iendayo kwenye mti wa uzima.#Ez. 10:22.
Zvasarudzwa nguva ino
1 Mose 3: SRB37
Sarudza vhesi
Pakurirana nevamwe
Sarudza zvinyorwa izvi
Unoda kuti zviratidziro zvako zvichengetedzwe pamidziyo yako yose? Nyoresa kana kuti pinda
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.