1
1 Mose 3:6
Swahili Roehl Bible 1937
Mwanamke alipoutazama huo mti akauona kuwa mwema wa kula, hata wa kuyapendeza macho, tena akauona, ya kuwa unapasa kutamaniwa kwa kuerevusha; ndipo, alipochuma tunda mojamoja, akala, akampa hata mumewe, naye akala.
Yenzanisa
Ongorora {{vhesi}}
2
1 Mose 3:1
Nyoka alikuwa mjanja kuliko nyama wote wa porini, Bwana Mungu aliowafanya. Naye akamwambia mwanamke: Kumbe Mungu amewakataza kuila miti yote iliyomo humu shambani?
3
1 Mose 3:15
Na niwachochee, mchukizane, wewe na huyu mwanamke, uzao wako na uzao wake, huyo atakuponda kichwa, nawe utamwuma kisigino.
4
1 Mose 3:16
Kisha akamwambia mwanamke: Nitakupatia maumivu mengi, utakapopata mimba, itakuwa kwa machngu mengi, ukizaa watoto; ijapo yawe hivyo, utamtamani mumeo, naye atakutawala.
5
1 Mose 3:19
Kwa jasho la uso wako utakula chakula, mpaka utakaporudi mchangani, kwani ndimo, ulimochukuliwa, kwani ndiwe mavumbi wewe, nayo mavumbi ndiyo, utakayokuwa tena.
6
1 Mose 3:17
Adamu naye akamwambia: Kwa kuwa umeiitikia sauti ya mkeo, ukaula ule mti, niliokuagiza kwamba: Usiule! nchi imeapizwa kwa ajili yako, uile na kuona uchungu siku zako zote za kuwapo.
7
1 Mose 3:11
Akasema: Ni nani aliyekuambia, ya kuwa wewe u mwenye uchi? Hukuula ule mti, niliokukataza, usiule?
8
1 Mose 3:24
Ndiyo sababu, aliyomfukuzia Adamu, nao upande wa maawioni kwa jua wa shamba la Edeni akaweka Makerubi wenye panga zimulikazo moto pande zote, wailinde njia iendayo kwenye mti wa uzima.
9
1 Mose 3:20
Adamu akamwita mkewe jina lake Ewa, kwa kuwa ndiye mama yao wote walio hai.
Pekutangira
Bhaibheri
Zvirongwa
Mavideo