Logo YouVersion
Ikona Hľadať

Marko MT. 1

1
1Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu; 2kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii,
Angalia, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako,
Atakaefanyiza njia yako mbele yako.
3Sauti yake aliae jangwani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Nyosheni mapito yake.
4Akatokea Yohana, akibatiza jangwani, na kuukhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. 5Wakamwendea inchi yote ya Yahudi, nao wa Yerusalemi, wakabatizwa nae katika mto Yardani, wakiziungama dhambi zao. 6Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kimioni mwake, akila nzige na asali ya mwitu. 7Akakhubiri akinena, Yuaja nyuma yangu aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba sistabili kuinama na kuzifungua kanda za viatu vyake. 8Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu.
9Tena, siku zile, alikuja Yesu kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yardani. 10Marra akapanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kwa mfano wa hua, akishuka juu yake; 11sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae.
12Marra Roho akamwongoza hatta jangwani. 13Akawako huko jangwani siku arubaini, akijaribiwa na Shetani; nae alikuwa pamoja na nyama wakali, na malaika walikuwa wakimkhudumia.
14Hatta baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiikhubiri injili ya ufalme wa Mungu, 15akineua, Wakati umetimia, na ufalme wa Muugu umekaribia; tubuni, kaiaminim injili.
16Nae akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simon na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. 17Yesu akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
18Marra wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 19Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. 20Marra akawaita: wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata.
21Wakashika njia hatta Kapernaum; na siku ya sabato akaingia sunagogi, akafundisha. 22Wakashangaa kwa mafundisho yake; kwa sababu alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka wala si kama waandishi. 23Palikuwapo katika sunagogi yao mtu mwenye pepo mchafu; akapaaza sauti, 24akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu. 25Yesu akamkaripia, akinena, Fumba kinywa, umtoke. 26Yule pepo mchafu akamrarua, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. 27Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii! 28Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya. 29Marra walipotoka katika sunagogi, wakalika nyumbani kwa Simon na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. 30Mama wa mkewe Simon alikuwa kitandani, hawezi homa; 31marra wakamwambia khahari zake: akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawakhudumia.
32Hatta ilipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, wakamletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. 33Na mji wote nlikuwa umekusanyika mlangoni. 34Akaponya wengi waliokuwa na maradhi nyingine nyingine, akafukuza pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
35Hatta alfajiri na mapema sana, akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipo watu akasali huko.
36Simon ua wenziwe wakamfuata; 37wakamwona, wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. 38Akawaambia, Twende pengine hatta vijiji vilivyo karibu, nipate kukhubiri na huko; maana kwa hiyo nalitokea. 39Akawa akikhubiri katika masuuagogi yao, katika inchi yote ya Galilaya, na kufukuza pepo.
40Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. 41Yesu akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. 42Marra hiyo ukoma wake ukamwondoka, akatakasika. 43Akamkataza kwa nguvu, marra akamwondosha, akamwambia, Fahamu, usimpe khabari mtu ye yote, 44bali enenda zako ukajiouyeshe kwa kuhani ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, illi kuwa ushuhuda kwao. 45Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.

Aktuálne označené:

Marko MT. 1: SWZZB1921

Zvýraznenie

Zdieľať

Kopírovať

None

Chceš mať svoje zvýraznenia uložené vo všetkých zariadeniach? Zaregistruj sa alebo sa prihlás