YouVersion Logo
Search Icon

Kutorokea MisriSample

Kutorokea Misri

DAY 4 OF 7

Kupigana na dhambi

Misri inaweza kuwa pahali pa kutorokea wakati wa shida. Lakini pia misri yaweza kuwa mfano wa kurudi kataika maisha ya dhambi. Mara nyingi tunapata kuwa wakristo wanakuwa na nguvu ya kiroho, lakini kwa wengi, hiyo haidumu sana. Wasipo na imani ya kutosha huwa wanarudi katakia maisha ya dhambi waliokuwa wakiishi kabla ya wokovu. Na hii inakuwa kawaida kwa wengi. Kuwa na nguvu halafu punde si punde kuteleza tena. 

Kama tu wana wa Israeli walipokuwa wafungwa misri, dhambi hutufanya kuwa wafungwa na kila mara tunapojaribu kuepuka, watawala wa watumwa hutulazimu tuishi katika hiyo hali.

Katika somo la leo cha Zaburi 18:2, tunapata kuwa kuna matumaini ya kuepuka maisha ya dhambi, kwani Bwana ndiye pekee yeye anayeweza kutukomboa kutoka katika maisha ya dhambi kwani yeye ndiye mwamba wa ukombozi wetu.  

Ombi la leo ni Bwana kutusaidia ili tugundue ya kwamba ni yeye peke anaye uwezo wa kutukomboa kutoka kwa maisha ya ufungwa misri.

 

Day 3Day 5

About this Plan

Kutorokea Misri

Muda mfupi baada ya ziara ya Wayahudi, ambao walijua kwamba Mfalme Herode alitaka kuua watoto wa eneo hilo, malaika alimtokea Yosefu katika ndoto kumwambia aende Misri na Maria na mtoto wa kijana Yesu. Swali 1: Ni nini unafikiri kinafanya watu watende kwa Yesu kama vile Herodi alitenda na kujaribu kumangamiza Yesu?  Swali 2: Kama vile Mungu alivyomlinda Yusufu na jamaa yake, je, anatulinda kwa njia gani siku hizi?  Swali 3: Unaweza kuelezea kuhusu wakati Mungu alikuhifadhi katika hali ngumu?

More