YouVersion Logo
Search Icon

Kutorokea MisriSample

Kutorokea Misri

DAY 3 OF 7

Mwamba Uliyo Juu Kuniliko

Moyo wa Maria ulipinga haraka sana. Alikua hajawahi kuwa na aina yoyote ya upasuaji. Na sasa alikuwa katika chumba cha kusubiri akisubiri daktari aje azungumze na wazazi wake kabla ya kuanza. Kulikuwa na vitu vingi ambavyo Maria hakua anaelewa, sanasana kinachomtendekea. Alikuwa na hofu sana. Baba yake alimshika mkono na kuzungumza naye kujaribu kumsaidia kujisikia vizuri zaidi. Alikuwa na Biblia yake pamoja naye na akafungua Zaburi ya 61 na kumsomea mistari 1-4. Alimkumbusha jinsi Mungu amemtunza sana na ataendelea kufanya hivyo kupitia upasuaji. Baba wa Maria alimkumbusha kuhusu wakati fulani katika maisha yake wakati alikuwa kijana mdogo na alipougua na ugonjwa wa kifuko. Mama yake na baba waliomba pamoja naye na Bwana akamsaidia kupitia upasuaji. Wakati mwingine tunaweza kuwa na hofu sana, lakini kwa sababu sisi ni wa Bwana tunaweza kumlilia. Tunajua kwamba Yeye husikia na hujali sana juu yetu. Yeye ndiye mwamba ulio juu kuliko sisi. Tunaweza kuchukua makao chini ya mabawa Yake katika nyakati ngumu, kama vile vifaranga hujificha chini ya mabawa ya mama yao wakati wa dhoruba zenye kutisha. Alimkumbusha Maria kwamba haifai hofu kwa sababu imani yake iko ndani ya Bwana. Je, si ni nzuri kwamba tunaweza kumwita Bwana wakati wowote tunamhitaji? Leo kataka jambo unalolipitia sahii, muambie bwana aje aingilie, kwani yeye ni mwamba iliyo juu.

Day 2Day 4

About this Plan

Kutorokea Misri

Muda mfupi baada ya ziara ya Wayahudi, ambao walijua kwamba Mfalme Herode alitaka kuua watoto wa eneo hilo, malaika alimtokea Yosefu katika ndoto kumwambia aende Misri na Maria na mtoto wa kijana Yesu. Swali 1: Ni nini unafikiri kinafanya watu watende kwa Yesu kama vile Herodi alitenda na kujaribu kumangamiza Yesu?  Swali 2: Kama vile Mungu alivyomlinda Yusufu na jamaa yake, je, anatulinda kwa njia gani siku hizi?  Swali 3: Unaweza kuelezea kuhusu wakati Mungu alikuhifadhi katika hali ngumu?

More