YouVersion Logo
Search Icon

Uvumilivu, Tunda La RohoSample

Uvumilivu, Tunda La Roho

DAY 5 OF 5

Uvumilivu dhidi ya Haki

Hadithi ya Biblia: Manna na kware - Kutoka 16: 1-18

Kifungu cha Mada: Yakobo 5: 8-9

Wanafunzi, wiki hii mechi ya kupigana nayo ni dhidi ya kujitakia. Kujitakia ni wakati pale mtu anaamini yakuwa anahitaji mapendeleo maalum, na wanakuwa wajeuri kuyahusu. Hii inaonekana kwa mataifa wenye pesa pale ambapo mtu anataraji yakuwa anafaa kuwa na kila kitu ambacho anataka ama anahitaji. Kujitakia pia kunaonekana kwa mataifa maskini palewanahisi ni haki yao kuomba kwa sababu wanafaa kupewa kama hao wengine.hakuna mtazamo mzuri kwa hayo mawili.

Mungu anataraji tuwe na uvumilivu na tuamuamini na maisha yetu.

Kwenye hadithi yetu yaleo , watu wa Israeli walijipata katika eneo la kuhitaji,na wakaanza kuomba na kulilia Mungu. Bibilia inasema kuwa walinungunika kwa Mungu, na wakateta wakisema wanahisi nikama wangekaa misri badala ya kufuata Mungu kwenye jangwa. Walipiga kelele na wakahisia heriwangekufia misri.lakini kisicho tarajiwa kilifanyika!m Mungu aliwachunga kimiujiza, kuwaumia maana na tombo kutoka angani! Kila asubuhi kulikuwa na mkate wa kula, kipande chembamba kiitachwo manna. Kwa kuongezea kila jioni kulikuwa na nyama ya kula, ndege waitwao tombo Mungu akiwatuma njia yao.

Lakini, hadi baada ya Mungu kuwafanyia miujiza hii, waliendelea kulia. Kwenye nambari 11:6, watu wa Israeli waliteta, “lakini sasa tumepoteza hamu yetu ya kula; hatuoni kitu kingine isipokuwa manna!”

Mungu alikasirikia wanaisraeli kwa kunungunika kwao na kuteta.walikuwa na hisia na kujitakia, pale walihisi yakuwa wanaweza dai vitu kutoka kwa mungu. Hakuna mmoja wetu anafaa kuitisha kitu kutoka kwa mtu.

Hatuwezi dai vitu kutoka kwa mungu, serikali zetu, wazazi wetu, kutoka kwa makanisa yetu, kutoka kwa wageni. Tunafaa kuwa na uvumilivu badala ya hisia ya kujitakia.

Maswali:

1. Ni vitu gani tunafaa kutarajia kutoka kwa serikali zetu?

2. Watu husema nini sana wakati wanateta na kulia kuhusu kile ambacho hawana?

3. Ushai kuwa na tama ya kudai kitu kutoka kwa mungu?

Maombi ya Maisha:

Wiki hii hudaiwi na mtu chochote. Kila wakati unataka kuomba kitu, jizuie mwenyewe. Kila wakati unapo jizuia mwenyewe kutoka kuomba chakula, kibali, wakati, au msaada; unapata ushindi dhidi ya dhambi hii.

Unataka nyongeza?

Mpango huu wa masomo wa siku tano ni vita vya UVUMILIVU dhidi ya kukosa subira, huzuni, kiburi, hasira, na kujiona kuwa mwadilifu. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia sura ya 5 kama mwongozo wa kututia moyo kutenda na kuwa mabingwa wa UVUMILIVU katika maisha yetu ya kila siku. Fuata kiungo ili kupata nyenzo za kanisa lako au kikundi cha vijana.

https://www.childrenareimportant.com/swahili/champions/

Day 4

About this Plan

Uvumilivu, Tunda La Roho

Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa siku tano wa kusoma unaonyesha vita vya UVUMILIVU dhidi ya kukosa subira, huzuni, kiburi, hasira, na kuhisi kuwa na haki. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UVUMILIVU katika maisha yetu ya kila siku.

More