Uvumilivu, Tunda La RohoSample
Uvumilivu dhidi ya Kiburi
Hadithi ya Biblia: Mfalme nebukadneza - Danieli 4
Kifungu cha Mada: Mhubiri 7:8
Leo tunajifunza kuhusu kiburi na jinsi gani inaweza kutushusha chini. Kwa kweli, kiburi inaweza kutuangamiza kabisa kama tukiruhusu! Ukweli ni kwamba tunapaswa daima kutambua kwamba Mungu ndiye ametusaidia kufanikisha chochote tunacho, na Anastahili kupata sifa zote. Vile tunajivuna katika mafanikio yetu wenyewe, ndivyo tunajipata kwenye shida zaidi.
Leo hadithi ya Biblia ni kuhusu mfalme Nebukadreza aliyekuwa amesimama juu ya paa lake, akitazama nje katika utawala wake wa ajabu. Akafikiria mwenyewe, "Ni mji mkuu wa ajabu wa namna gani nimejitengenezea mwenyewe," kimsingi ni kusema, "Mimi ni mkuu sana!" Mungu alimwonya mfalme huu mwaka uliotangulia katika ndoto kuwa makini kuhusu kiburi, au Mungu mwenyewe atamyenyekeza. Hata hivyo, yeye alikuwa pale amesimama juu ya dari lake, amejaa kiburi kwa yote aliyokuwa amefanikisha. Hivyo Mungu akamyenyekeza.
Maneno bado yalikuwa kwenye midomo ya mfalme wakati sauti inatoka mbinguni kuchukua mamlaka. Alifukuzwa mbali na ikulu, na kupoteza akili zake. Yeye akatangatanga misituni nje ya mji kama ng'ombe huku nywele zake na kucha zikiwa refu. Huyu mfalme maarufu akawa na maisha ya wanyama pori peke yake nje.
Kiburi ni dhambi mbaya, na Mungu hana uvumilivu kwa hilo. Mungu anaweza kunyenyekeza watu, kuchukua kazi zao za ajabu au kusababisha kupoteza fedha. Mungu ni mkuu na Yeye anatujali. Wakati tunapatikana na kiburi, ni kwa maslahi yetu bora kwamba Mungu anatunyenyekeza. Kwa upande mwingine, tunaweza kufanya maisha rahisi kwa kunyenyekea wenyewe kabla Yeye kufanya hivyo.
Kiburi ni adui dhidi ya tunda la roho. Mwezi huu tunajifunza kuhusu uvumilivu. Inaweza kuwa vigumu sana kusubiri. Wakati mwingine inabidi kusubiri Mungu kutimiza ndoto Alioahidi, au sisi kusubiri wengine kufanya kile walivyoahidi. Aidha, kiburi inaweza kupitia njia yetu ya uvumilivu. Jinsi tunavyojihisi kuwa juu, ndivyo tunakosa kusubiri wengine. Mfalme hapaswi kusubiri mtu yeyote! Hivyo tunavyojiona kama wafalme, ndivyo tunakosa subira. Biblia inasema kwamba mfalme huyu aliishi kama mnyama kwa “mara" 7, ambayo inamaanisha miaka 7! Baada ya muda huo, Nebukadreza akatazama juu mbinguni na akakubali kuwa Mungu alikuwa mfalme halisi duniani, naye akamsifu Mungu na kumpa utukufu. Akili zake zikarudi kwake, naye akarejeshewa ufalme.
Je, unataka kunyenyekezwa na Mungu, au kujinyenyekeza mwenyewe? Chaguo ni lako.
Maswali:
1. Je, unafikiri mfalme kweli aikuwa wazimu na kula nyasi?
2. Inakuwaje mfalme kuwa alijinyenyekeza mwenyewe bila Mungu kuhusika?
3. Je, watu wanajiona wafalme vipi katika jamii yako? Na inaonekana aje?
Maombi ya Maisha:
Fanya shughuli kadhaa kujinyenyekeza. Unaweza kumpa mtu nafasi yako katika mstari, epuka kutazama kipinda katika runinga ambapo wahusika wamejaa kiburi, peana sehemu yako katika jukwaa au mbele ya wengine, au ruhusu wengine kuwa sahihi.
About this Plan
Je, tunda la roho linawezaje kushinda vita dhidi ya dhambi za mwili wangu? Mpango huu wa siku tano wa kusoma unaonyesha vita vya UVUMILIVU dhidi ya kukosa subira, huzuni, kiburi, hasira, na kuhisi kuwa na haki. Kristi Krauss anatumia tunda la roho linalopatikana katika Wagalatia mlango wa 5 kama mwongozo wa kutuhamasisha kutenda na kuwa mabingwa wa UVUMILIVU katika maisha yetu ya kila siku.
More