Wimbo Wa NeemaSample
Mungu yuko wapi wakati maisha yanapokuwa magumu?
Kama umewahi kujiuliza hivi, basi uko katika jamii nzuri. Nimejiuliza swali hilohilo. Vilevile kila binadamu yeyote. Mambo yanapobadilika katika maisha yako - unapopitia vikwazo kila mahali - tunalia, " Uko wapi, Mungu?"
Na jibu linalotujia ni jibu bora sana ambalo utawahi kusikia.
Warumi 8:38-39 inasema,
"Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka,wala yaliyopo, wala yatakapokuwako, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Sawa, Kulingana na kifungu hicho, Mungu yuko wapi maisha yanapokuwa magumu? Yuko wapi marafiki wako wanapokuacha? Au familia yako inapovunjika? Au ndoto zako zinapokosa kutimia?
Biblia inasema kwamba Mungu yuko pamoja na wewe wakati wa shida - anakupenda katika yote.
Sasa, unaweza kufikiri, "Vizuri... Lakini mbona haniondolei shida zangu?"
Swali nzuri. Hilo ni swali lingine ambalo watu wengi wameuliza. Kama mtume Paulo, ambaye aliandika kifungu hicho hapo juu.
Paulo alivumilia machungu ya moyo na magumu mengi sana katika miaka michache na mifupi kuliko miaka ambayo watu hupitia katika maisha yao. Alipigwa, akadhihakiwa, akavunjwa moyo, na kufungwa gerezani. Alipoteza marafiki kupitia kifo, akawa mpweke na kupigana na mfadhaiko. Mwishowe, Paulo mwenyewe aliuawa kwa Kumfuata Yesu.
Wakati mmoja, Paulo alikuwa anapitia wakati mgumu sana. Hatujui alikuwa anapitia nini, lakini aliifafanua kama mwiba ndani ya mwili wake. Labda ulikuwa ugonjwa, ugonjwa wa kiakili, au maumivu sugu.Chochote kile, hakuweza kukiondoa, na akamuomba Mungu amwondolee.
Mungu akamjibu…
"Neema yangu yakutosha, maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu."( 2 Wakorintho 12:9)
Je, Mungu anamaanisha nini? Je, hajali kuwa Paulo anateseka?
Anajali kabisa. Kama vile anavyojali kuhusu shida zako za maisha. Usisahau kuwa Yesu alikuwa binadamu " anayejua shida" kama inavyosema Isaya 53:3. Anajua majonzi. Anatuelewa. Anakupenda.
Lakini kile ambacho mimi na wewe tunahitaji sana - na kile ambacho dunia hii inahitaji sana - sio kubadilika kwa mambo, bali ni mabadiliko ya kiroho.
Hivyo ndivyo anavyofanya Yesu Anapokuja katika maisha yako. Na hilo ndilo tumaini Analoonyesha katika maisha yako anapokusaidia kupitia katika maumivu badala ya kukutoa katika maumivu hayo.
Anasema, "Nitakusaidia kupitia haya. Nitakufinyanga kupitia haya. Nitakutumia kuonyesha neema yangu kwa dunia inayonihitaji mimi kuliko chochote kile."
Kwa hivyo magumu yoyote, machungu ya moyo, maumivu unayopitia leo, upate amani katika ahadi ya Mungu kwamba Hatakuacha, hakuna kinachoweza kukutenganisha na upendo wake kwa Yesu, na unachohitaji ni neema yake tu. Na hivyo utaweza kuimba kwa imani…
Kilikuwa mwenye hofu,
Nilifungwa nazo,
Nimefunguliwa sasa,
Kwa neema ya Yesu.
Baraka,
—Nick Hall
About this Plan
Gundua undani wa upendo wa Mungu kwako kupitia ibada hii ya Wimbo wa Neema. Mwinjilisti Nick Hall atakuongoza kupitia ibada yenye nguvu ya siku 5 akikualika kujiunga na Wimbo wa neema ya Mungu unaoimbwa juu yako.
More