Wimbo Wa NeemaSample
Kitu ninachokipenda sana kuhusu kumfuata Yesu ndicho nisichokipenda kabisa kuhusu kufuata Yesu.
Acha nieleze…
Napenda kuwa Mungu alinikaribisha katika familia Yake. Sikustahili yote hayo. Nilichostahili ni hukumu ya dhambi za maisha yangu, na hakuna kile ambacho ningefanya ili kurekebisha. Ni kama nimeshindwa kuingia katika klabu… gharama yake ilikuwa juu sana...halafu Mungu akaingia kati na kunilipia.
Hio ni neema.
Lakini, neema ya Mungu ni ya kila mtu, wakiwemo watu ambao hufanya maisha yako yawe magumu.
Sisi wote tuna watu katika maisha yetu ambao hutuvunja moyo, kutukosea, na kutukasirisha. Labda ni mtu ambaye unamjua. Au labda ni mtu kwenye mtandao.
Mara nyingi sana katika dunia ya leo, watu ambao hutusumbua sana ni watu ambao hata hatujawahi kukutana nao; mtu mashuhuri, chama cha kisiasa, mtu anayevutia watu kwenye TikTok.
Yeyote yule, ni jambo la kawaida kwamba mtu anapotukosea, wanakuwa "wao."
Kwamba, huwezi kuwaelewa. Huwezi kuzungumza nao. Huwezi kuwaheshimu. Huwezi kuwapenda.
Wanadamu wana tabia ya kujua na kukashifu watu - mara nyingi ni vikundi vya watu- kwa kutumia njia ambazo hatuwezi kuzitumia kujihukumu sisi wenyewe. Mimi huhukumu. Najua vilevile wewe huhukumu pia.
Sifa kwa Mungu kwa sababu Yeye hahukumu!
Kwa sababu,cha muhimu kuhusu neema ni kuwa tunaihitaji sisi wote. Na tunapoipokea, Mungu anakuita wewe na mimi ili tuendeleze neema yake ya ajabu kwa wengine.
Wakolosai 3:13 inasema,
"Mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo ninyi."
Mungu hakuwa na deni la upendo wake kwangu. Hakuwa na deni la msamaha. Hakuwa na deni la uhusiano wake na mimi au ahadi ya uzima wa milele mbinguni. Yote hayo ni neema tu. Kwa hivyo swali ambalo lazima tujiulize ni: tunawezaje kupokea neema ya ajabu ya aina hii kutoka kwa Mungu na tukose kuitoa kwa wengine?
Neema haimanishi ukubaliane na kila kitu ambacho mtu anasema au anafanya. Neema haimaanishi kuwa utupilie mbali dhambi duniani. Neema haimanishi kuwa usisimame imara katika ukweli.
Neema inamaanisha kuwa haumkashifu mtu au kukosa kumpenda kwa sababu alikukosea au hata kukufanyia mabaya. Kwa nini?
Kwa sababu hivyo ndivyo Mungu anavyokupenda… na hivyo ndivyo Mungu anavyowapenda.
Baraka,
—Nick Hall
Scripture
About this Plan
Gundua undani wa upendo wa Mungu kwako kupitia ibada hii ya Wimbo wa Neema. Mwinjilisti Nick Hall atakuongoza kupitia ibada yenye nguvu ya siku 5 akikualika kujiunga na Wimbo wa neema ya Mungu unaoimbwa juu yako.
More