INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILISample
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15962%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
KUFUFUKA KWA YESU
MATTHEW 28
2 Ghafula pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni akaenda penye kaburi akalivingirisha lile jiwe na kulikalia.
3 Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. ya huyo malaika ilikuwa kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
MARK 16
1 Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo na Salome
walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.
4 Lakini walipotazama, wakaona lile jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha kuvingirishwa kutoka pale penye ingilio la kaburi.
5 Walipokuwa wakiingia mle kaburini, wakamwona kijana mmoja aliyevaa joho jeupe akiwa ameketi upande wa kuume, nao wakastaajabu.
6 Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza.
7 Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro, kwamba ‘Anawatangulia kwenda Galilaya, huko ndiko mtakakomwona, kama alivyowaambia.’ ”
LUKE 20
3 Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara kuelekea kaburini.
4 Wote wawili walikuwa wanakimbia, lakini yule mwanafunzi mwingine akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.
5 Alipofika, akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani vilivyokuwa sanda mle ndani, lakini hakuingia.
6 Ndipo Simoni Petro akaja, akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini
7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda.
8 Kisha yule mwanafunzi aliyetangulia kufika kaburini naye akaingia ndani, akaona, akaamini,
9 (kwa kuwa mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale maandiko kwamba ilikuwa lazima Yesu afufuke kutoka kwa wafu).
10 Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.
Scripture
About this Plan
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15962%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More