YouVersion Logo
Search Icon

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILISample

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

DAY 2 OF 7

MAOMBI KWENYE BUSTANI KUSALITIWA NA KUKAMATWA

LUKE 22

Aliporudi kwa wanafunzi wake, akawakuta tena wamelala, kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia.

Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazama, Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.Amkeni! Twendeni zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”

"Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja, ukiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu.Lakini Yesu akamwambia,"

“Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema,

“Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” Mmoja wao akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.Lakini Yesu akasema,

“Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

MATTHEW 26

Wakati huo Yesu akawaambia ule umati wa watu, 

“Mmetoka na panga na marungu kuja kunikamata kama vile mimi ni mnyang'anyi? 

Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata?

Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” 

Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Day 1Day 3

About this Plan

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More