Zaburi 5
5
Mwamini Mungu kwa ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji: kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.
1Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu,
Ukuangalie kutafakari kwangu.
2Uisikie sauti ya kilio changu,
Ee Mfalme wangu na Mungu wangu,
Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.
3 #
Zab 30:5
BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,
Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
4 #
Mal 2:17
Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;
Mtu mwovu hatakaa kwako;
5 #
Zab 14:1; Hab 1:13 Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako;
Unawachukia wote watendao uovu.
6Utawaharibu wasemao uongo;
BWANA humchukia mwuaji na mwenye hila
7 #
1 Fal 8:29
Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako,
Nitaingia nyumbani mwako;
Na kusujudu kwa kicho,
Nikilielekea hekalu lako takatifu.
8BWANA, uniongoze kwa haki yako,
Kwa sababu yao wanaoniotea.
Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,
9 #
Rum 3:13
Maana vinywani mwao hamna uaminifu;
Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi,
Ulimi wao hujipendekeza.
10Wewe, Mungu, uwapatilize,
Na waanguke kwa mashauri yao.
Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao,
Kwa maana wamekuasi Wewe.
11 #
1 Kor 2:9
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi;
Watapiga kelele za furaha daima.
Kwa kuwa Wewe unawahifadhi,
Walipendao jina lako watakufurahia.
12Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki;
BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.
Atualmente Selecionado:
Zaburi 5: SRUV
Destaque
Compartilhar
Copiar

Quer salvar seus destaques em todos os seus dispositivos? Cadastre-se ou faça o login
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.